Gilgal Revival Church (G.R.C) ni huduma iliyojengwa kwa kufuata maandiko matakatifu yaani BIBLIA, nakuamini juu ya wokovu kamili kupitia Bwana wetu Yesu Kristo.
Huduma hii ilianzishwa mnamo mwaka Tarehe 01 mwezi Julai mwaka 2017, chini ya Askofu Mkuu Bishop Paul Israel Shabani,Ilianza ikiwa huduma/kanisa la Mahali pamoja Jijini Dar es salaam, Lakini sasa imeenea na matawi yake katika kanda zote Tanzania na Nje ya mipaka ya Tanzania.
Huduma hii imelenga kuhudumia watu kiroho bila kubagua haiba wala asili ya mtu,
Watu wote wenye uhitaji wa kiroho wanafikiwa kwa utaratibu maalumu ambapo upo ndani ya katiba
ya Kanisa.
Tunatoa huduma kwa jamii na kuigusa
moja kwa moja hasa kwa watu walio ndani ya jamii wenye uhitaji mbalimbali mfano:Wajane ,Yatim ,Wasiojiweza Wafungwa
Karibu Ujumuike nasi katika Kumsifu na Kumuabudu Mungu
Angalia Mahubiri yetu youtube
Tunakukaribisha Ujifunze zaidi kupitia Chaneli yetu ya Youtube
Unahitaji Maombi?
Maisha yanaweza kuwa magumu wakati mwingine, na sote tunahitaji maombi. Tunachukua ombi lako kwa uzito mkubwa, na haijalishi unachopitia, tungependa kuomba pamoja nawe!"